Sunday, December 14, 2014

EPL: KILICHOWAKUTA LIVERPOOL VS MAN UNITED HIKI HAPA

IMG_9861.JPG
MICHUANO ya ligi kuu ya Uingereza imeendelea tena jioni ya leo kwa mchezo wa mahasimu wa jadi Liverpool dhidi ya Manchester United.
Mchezo huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka ulimwenguni umemalizika hivi punde katika uwanja wa Old Trafford.
Magoli ya Wayne Rooney katika dakika ya 10 ya mchezo, Juan Mata dakika ya 40 yaliwapeleka United mapumziko wakiwa kifua mbele kwa 2-0.
Kipindi cha pili Liverpool walijaribu kusawazisha lakini jitihada zao ziliishia mikononi mwa kipa David De Gea.
Robin van Persie alifunga la tatu na la ushindi kwa timu yake na kuweka rekodi ya kushinda mechi 6 mfululizo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI