Thursday, November 13, 2014

ZAIDI YA WAHUDUMU 400 WA HOSPITALI WAFANYA MGOMO NCHINI SIERA LEONE

Zaidi ya wahudumu 400 wa afya wanao watibu wagonjwa wa Ebola katika kliniki moja nchini Sierra Leone wamegoma.
Wahudumu hao wakiwemo wauguzi na wafanyakazi wengineo wanagoma kushinikiza kuwalipa dola miamoja kila wiki kwa kuhatarisha maisha yao kutokana na kuwashughulikia wagonjwa wa Ebola.
Kliniki hiyo iliyo mjini Bandajuma karibu na eneo la Bo, ni kliniki pekee ambayo wagonjwa wa Ebola wanatibiwa Kusini mwa Sierra Leone.
Kwingineko nchini Mali, muuguzi mmoja pamoja na mgonjwa aliyetibiwa na muuguzi huyo wamefariki kutokana na ugonjwa wa Ebola.
Idadi hiyo inafikisha watu watatu waliofariki kutokana na Ugonjwa huo nchini Mali.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, idadi ya watu waliofariki duniani kutokana na mfumuko wa ugonjwa wa homa ya Ebola huko Magharibi mwa Afrika imeongezeka na kufikia 5,147 huku watu wengine 14,068 wakiambukizwa ugonjwa huo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI