JESHI LA POLISI la Kenya limetangaza kuwa limewatia nguvuni wapiganaji 10 wa kundi la al Shabab la Somalia wakiwemo wanawake wawili waliokuwa na nia ya kujilipua kwa mabomu.
Mkuu wa Polisi ya Kenya David Kimaiyo ambaye ameongeza kuwa maafisa wa polisi wamewakamata washukiwa hao waliokuwa na mpango wa kufanya mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya kupitia ripoti za kiintelijensia.
Kimaiyo ambaye hakueleza washukiwa hao walikamatwa lini amesema washukiwa hao walihusika na mashambulizi kadhaa ya kigaidi mjini Nairobi na kutorokea nje ya nchi.
Mkuu huyo wa polisi anasema kuwa kwa sasa washukiwa hao kumi wanaendelea kuhojiwa na maafisa wa usalama ili kubaini iwapo kuna wengine na baada ya uchunguzi kukamilika wata funguliwa mashtaka.
Kenya imekumbwa na mashambulizi ya kigaidi katika miezi ya hivi karibuni ambayo yanahusishwa na kundi la kigaidi la al Shabab.
Kundi hilo lilidai kuwa ndilo lililohusika la shambulizi la Septemba 2013 dhidi ya jengo la maduka la Wastgate jijini Nairobi ambalo lilisababisha mauaji ya watu wasiopungua 67.
0 comments:
Post a Comment