Shirikisho la soka nchini Urusi limesema, Mkufunzi wa timu ya Rostov, Igor Gamula amesimamishwa kazi kwa kipindi cha wiki tano baada ya kupatikana na hatia ya kutoa maoni ya kibaguzi.
GAMULA aliadhibiwa baada ya kueleza wanahabari kuwa klabu yake ina ''wachezaji wenye ngozi ya rangi nyeusi wa kutosha,tuna sita ya aina hiyo.''
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 54 ameomba radhi kwa kila mmoja wa wachezaji hao.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa kusudi ya maongezi yake ilikuwa utani. Kwani ana uhusiano mkubwa na wachezaji wote wenye ngozi nyeusi. Hivyo Vyombo vya habari vya Uingereza havi elewi utani wa Warusi.
Hata hivyo Waziri wa michezo Afrika Kusini, Fikile Mbalula na Rais wa Shirikisho la soka nchini humo Danny Jordaan wameliomba shirikisho la soka duniani FIFA kuangalia kwa ndani maoni ya Gamula.
Walisema Nchi yoyote,inayotarajiwa kuwa mwenyeji wa maandalizi ya kombe la Dunia inafaa kuwa karimu kwa taifa na kabila lolote bila kubagua kwa misingi ya rangi ya ngozi yao na hasa Urusi.
Jordaan aliongeza kuwa aamini kuwa Gamula anafaa kupewa adhabu kali zaidi. Kwani Hii si mara ya kwanza mambo kama haya yamesemwa nchini Urusi.
0 comments:
Post a Comment