KUPITIA kipindi cha Kili Chat cha hivi karibuni, Wema alielezea kazi zake mpya za filamu anazotarajia kuzitoa hivi karibuni.
“Kwanza ntaanza kuitoa Supastaa, halafu kuna nyingine inaitwa ‘The Unexpected’ and then kuna nyingine ambayo nimefanya na Aunty, nimetoka kushoot juzi tu inaitwa Family. Kwahiyo nina kama movie tatu then kuna a very big project coming,” alisema Wema.
Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 pia anatarajia kuzindua msimu wa pili wa kipindi chake cha In My Shoes ambapo awamu hii atakuwa akionekana pia mpenzi wake, Diamond.
0 comments:
Post a Comment