Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu.
BAADA ya serikali kutoa siku saba za uchunguzi wa sakata la umri wa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, maamuzi ya uchunguzi huo yameendelea kuwa katika hali ya sintofahamu baada ya kila upande kuonekana kutokuwa tayari kuweka wazi juu ya kinachoendelea.
Wiki iliyopita, Naibu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma
Nkamia, alisema kuwa wametoa siku saba kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kufanya uchunguzi juu ya suala hilo lakini mpaka jana hakuna ripoti iliyokuwa imetolewa.
Nkamia, alisema kuwa wametoa siku saba kwa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kufanya uchunguzi juu ya suala hilo lakini mpaka jana hakuna ripoti iliyokuwa imetolewa.
Championi Ijumaa lilizungumza na Ofisa Habari wa Basata, Aristides Kwizela ambapo alisema uchunguzi wa suala hilo bado haujakamilika.
“Ni kweli siku saba zimepita lakini bado uchunguzi haujakamilika, hatuwezi kusema utakamilika lini ila ufafanuzi utatolewa tu,” alisema Kwizela.
0 comments:
Post a Comment