NESI Kaci Hickox akiendesha baiskeli baada ya kuvunja karatini aliyowekewa wakati akiwa kwenye uchunguzi wa Ebola baada ya kurudi toka Afrika Magharibi alipokua akiwatibu wagonjwa wa Ebola.
Mamlaka ya afya mji wa Fort Kent, Maine uliopo mpakani wa Canada wamesema watamfikisha mahakamani Nesi Kaci Hickox baada ya kuvunja karantini siku ya Alhamisi Oktoba 30, 2014 kwa kutoka nje ya nyumba yake na kuendesha baiskeli takribani saa moja.
Nesi Kaci Hickox aliwekewa karantini hiyo baada ya kurudi toka Afrika Magharibi alipokua amekwenda kuwatibia waathirika wa ugonjwa wa Ebola.
Pamoja na ulinzi wa polisi uliowekwa nje ya nyumba yake Nesi Kaci Hickox alithubutu kutoka nje ya nyumba yake kwa siku mbili mfulululizo baada ya siku ya Jumatano Oktoba 29, 2014 kutoka nje ya nyumba yake na kuongea na waandishi wa habari huku akishikana mkono na baadhi ya waandishi hao.
Nesi Kaci Hickox alitakiwa akae ndani ya nyumba yake kwa siku 21 mpaka Novemba 10.
0 comments:
Post a Comment