Friday, November 14, 2014

MSIBA WA MWAKA: VITUKO VYATAWALA MAZISHI YA MSANII MABOVU IRINGA, MLEVI AFANYA VURUGU KUBWA *PICHAZ*

Wasanii wakielezea kifo cha mabovu , Juu ni Msanii Mabovu enzi za uhai wake
Waombolezaji wakiwa na jeneza la msanii Mabovu kutoka msikiti wa Mwangata kwenda makaburi ya Mlolo Iringa
Wasanii wakiwa wamelipiga chata kaburi la mabovu mara baada ya mazishi yake
Baadhi ya wasanii wa kundi la Weusi ambao wamefika Iringa kumzika msanii Mabovu leo

Makini akichangisha rambi rambi
Msanii JOh Makini akiwa na michango ya msiba wa mwenzao Mabovu leo
Mwakilishi wa wasanii wa kundi la Weusi Joh Makini kushoto akimpa pore baba wa msanii Mabovu mzee Upete kulia baada ya kumaliza kuzika nyumbani kwake Mwangata wengine ni baadhi ya wasanii walioshiriki mazishi hayo leo
Mwakilishi wa kundi la weusi kwanza Joh Makini akizungumza na mtandao huu wa matukiodaima leo
Picha na habari na kikosi cha Matukio daima
Vituko vyatawala msiba wa msanii Ahmed Zubery Upete a. k. a Geez Mabovu Iringa mlevi (pichani aliyekaa chini)atembeza kichapo kwa wafiwa kisa ataka aruhusiwe kuufukua mwili wa marehemu ili auage Mara ya mwisho asisitiza kuwa marehemu amekua nae na ana siri nzito ya kifo chake.

Tukio hilo limetokea muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili makaburi ya Mlolo nje kidogo ya mji wa Iringa kwa mazishi.

Chapombe huyo ambae alifika makaburini hapo kwa kuchelewa alivamia eneo hilo la mazishi kwa kuanza kutoa lugha za matusi ya nguoni kwa wafiwa kwa madai wamewezaje kumzika marehemu huyo bila ya yeye kufika eneo hilo.

Kutokana na lugha hizo za matusi iliwalazimu Vijana waombolezaji kumtoa kwa nguvu eneo hilo na kwenda nae pembeni kidogo kumsihi asifanye vurugu kabla ya chapombe huyo kuanza kurusha Ngumi kwa wasanii.
Akizungumza mara baada ya mazishi hayo mmoja kati ya wadau wa tasinia ya muziki nchini na promota mkubwa wa mziki nyanda za juu kusini Edwin Bashir ambae ni mtangazaji wa kituo cha Radio Ebony Fm alisema kuwa mbali ya umoja ambao wasanii wameuonyesha katika msiba huo kwa kuja kushiriki mazishi ila bado angeshauri wasanii kwa wakati mwingine kujenga ushirikiano wa kumjulia hali mwenzao pindi anapoumwa.

” Sisemi kwa ubaya ila kiukweli msanii Geez Mabovu ameumwa sana karibu mwaka mzima anasumbuliwa na ugonjwa wake ila hakuna msanii ambae amefika kumjulia hali ila leo wengi wamesafiri kuja kumzika….. inapendeza kusaidiana wakati wa ugonjwa badala ya kusubiri mwenzenu afe “

Bashir alisema kuwa msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wa mwanzo zaidi kuutangaza mkoa wa Iriga katika tasnia ya muziki na kuwa hata kabla ya vituo vya radio kuanzishwa mkoani Iringa alikuwa akiutangaza mkoa na kusikika katika radio mbali mbali za nje ya Iringa.

Alisema kuwa msanii huyo toka amemaliza elimu yake kamwe hajapata kufanya shughuli nyingine nje ya mziki na kuwa wakati wote alikuwa akijishughulisha na muziki zaidi .

Hata hivyo alisema chanzo cha Mabovu kuhama mkoa wa Iringa na kuhamishia makazi yake jijini Dar es Salaam ni kuzidi kuutangaza muziki zaidi na mkoa wake wa Iringa malengo ambayo alipata kufanikiwa kwa kiasi kikubwa .

” Utaona jinsi ambavyo msiba wake leo ulivyowavuta watu wegi wapenzi na wadau wa muziki kutoka mikoa mbali mbali ya nje ya Iringa ambao kimsingi baadhi yao imekuwa ni mara yao ya kwanza kufika Iringa ….pamoja na kufarijika kwa umati wa watu waliofika kumzika ila moyo umeniuma sana hasa ukizingatia kuwa kifo chake hakikuwa na ghafla bali amekufa kwa mateso makubwa kwa kuugua karibu mwaka mzima sasa hivyo kwa umoja huo ningetegemea wangefika enzi za uhai wake kumuuguza mwenzao”

Kwa upande wake mwakilishi kwa kundi la Weusi Bw Joh Makini alisema kuwa kifo cha Mabovu kimeacha pengo kubwa katika tasnia ya muziki hasa muziki wa hiphop Tanzania,

Alisema kuwa Mabovu amepata kuishinae Kinondoni Jijini Dar es Salaam mtaa mmoja ila pia amepata kushirikiana kazi mbali mbali za kimzuki .

Hivyo alisema kuwa ushirikiano huo ndio ambao umewasukuma kufika mkoani Iringa kushiriki mazishi hayo baada ya pengo kubwa ambalo wamelipata .

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wazawa na mkoa wa Iringa msanii Squza,alisema kuwa Iringa imempoteza msanii mkongwe na kuwa kifo chake kitaenziwa na wasanii wa mkoa wa Iringa pia ambao wapo nje ya mkoa huo kwa kuangalia jambo la kufanya katika kuwanyanyua wasanii chipukizi wa mkoa huo.

Alisema kuwa wapo wasanii maarufu wengi kutoka mkoa wa Iringa ambao wana majina makubwa kama Rehema Chalamila (RAY C} akina MiKe T na wengine wengi na kuwa kama njia ya kumuenzi Mabovu watahakikisha wanaunganisha nguvu kwa kushirikiana na vyombo vya habari kuona Iringa inampata mwakilishi mwingine wa Mabovu kutoka kwa wasanii Chipukizi .

Msanii Mabovu alifariki dunia jana majira ya saa 2 usiku nyumbani kwa wazazi wake eneo la Mwangata mjini Iringa ambako alikuwa akiugulia na amezikwa leo katika makaburi ya Mlolo nje kidogo na mji wa Iringa

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI