Tuesday, November 4, 2014

MIUJIZI YA KARNE: SHEKH SHARIF KHAMIS WA TANZANIA AONYESHA MIUJIZA NDANI YA MELI...MANAHODHA PAMOJA NA ABIRIA WADUWAA!!! *PICHAZ*

Shekh Sharif Khamis hapa ndipo alipowaacha watu midomo wazi na mshangao baada ya kuendesha Meli wakati hajawahi kusomea urubani.
Maelfu ya wakazi wa mji wa Goma wakiwa kwenye muhadhara kumsikiliza miujiza ya uponyaji wa dua za Shekh Sharif Khamis.
Na Sharifa Abdalah- Bukavu Kongo
UKISIKIA hizi habari kwenye radio unaweza usiamini unaweza ukadhani ni kichekesho ama hadithi lakini ni kweli yametokea, kijana wa kitanzania Shekh Sharif Khamis ambae kadri anavyokuwa kiumri ndipo anazidi kufanya miujiza ya kipekee na ya kuogopesha.
Akiongea na Maskanibongotz mwandishi wetu aliyeko mji wa Bukavu Shekh Sharifu ambae kabla ya kutua nchini Kongo alikuwa nchi ya Uturki alikokuwa amepewa mwaliko na Serikali ya huko kwa ajili ya kwenda kufanya dua na huko nako alifanya maajabu. 
Hata hivyo kwenye tukio hilo la kuendesha meli ilikuwa  wakati wakiwa ndani ya Meli wakitokea mji wa Goma kwenda Bukavu ndipo kijana huyo alipomwambia nahodha wa meli hiyo kuwa anaweza kuendesha mtambo huo huku mamia ya watu wakishuhudia palitokea mabishano makubwa huku manahodha mbalimbali wakimwambia hawezi kuendesha meli hiyo kwa vile kama hajawahi kusomea uderva hawezi kufanya kitu kama hicho.
Baada ya mabishano ya muda mrefu nahodha wa meli hiyo iliyofahamika kwa jina la MV Emmanul alipompa nafasi Shekh huyo na katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana huyo alianza kusukuma mtambo huo huku kila mtu akipigwa na butwaa kwa tukio hilo na aliendesha kwa muda mrefu hadi kufika mji wa Bukavu na kutia nanga.
Kufuatia tukio hilo mamia ya watu walimuogopa Mungu kwa maajabu. hiyo huku manahodha wakisema huo ulikuwa ni maajabu. mkubwa na wengine wakishindwa kuamini kama kijana huyo ni binadamu wa kawaida ama ni maajabu.
Hata hivyo wananchi wa Kongo wamemuomba Shekh Sharif kuwafikishia shukrani zao kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwasaidia kwa kupeleka Majeshi nchini mwao.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI