WATU wawili wamepoteza maisha na maelfu kuyahama makazi yao kutokana na mafuriko yaliyotokea huko Argentina katika jimbo la Buenos Aires yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha tangu ijumaa.
Dhoruba , upepo mkali pamoja na mvua kubwa imesababisha mafuriko katika mji mkuu wa Argentina na kuwalazimu wakazi wa mji huo kuyahama makazi yao.
Mvua hiyo imesababisha barabara pamoja na majengo yaliyozunguka mji huo kuharibiwa vibaya.
Kufuatia Mafuriko hayo Viongozi wa serikali wamewapeleka askari wapatao 5000 kwa ajili ya kutoa misaada katika maeneo ambayo yameathirika zaidi.
Mvua kubwa zinazosababisha mafuriko zimekuwa ni tishio katika baadhi ya maeneo kaskazini mwa Agentina na katika baadhi ya Maeneo nchini Uruguay.
Kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa Nchini humo mvua hizo zinatarajia kumalizika hapo kesho katika mji wa Buenos Aires.
***Picha Zaidi***
0 comments:
Post a Comment