ZAMBIA imekuwa katika hali ya Mtikisiko baada ya kiongozi wa kwanza mweupe aliye Kaimu Urais Guy Scott kumuondoa madarakani katibu mkuu wa chama tawala, hivyo kuzua maandamano YA kuukataa utawala wake.
Wafuasi wa chama cha Patriotic Front ambacho kiongozi wake Edgar Lungu ameondolewa madarakani siku chache baada ya kifo cha Rais wa nchi hiyo Michael Sata walizunguka katika mji mkuu wa Lusaka na kuanza kurusha mawe katika magari na kuchoma miti.
Rais wa muda wa Zambia Guy Scott
Kwa mujibu wa Radio ya Taifa ya Zambia, Scott atakaye ongoza nchi hiyo yenye utajiri wa madini ya shaba katika siku 90 kabla ya uchaguzi amemfukuza Edgar Lungu kutofanya kazi za chama chake.
Lungu ambaye pia ni waziri wa ulinzi wa Zambia alichaguliwa na Sata kukaimu nafasi ya Sata wakati ambapo marehemu Sata mwenye umri wa miaka 77 alipokuwa anaondoka nchini humo kwaajili ya matibabu mwezi uliopita.
Marehemu Rais Sata.
Sata amefariki dunia Jijini London kwa ugonjwa ambao mpaka sasa hauja tambuliwa na mwili wake unatarajia kuzikwa tarehe 11 mwezi Novemba.
Katika mkutano wa baraza la mawaziri uliofanyika baada ya kifo cha Sata, Scott, aliteuliwa kuikaimu nafasi ya Urais , na kuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika mzungu kushika nafasi hiyo tangu ubaguzi wa rangi.
Rais Obama na mkewe walipokutana na Rais wa muda wa Zambia Guy Scott na mkewe.
Katika barua aliyoiandika tarehe 3 Novemba Scott alimfukuza Lungu ambaye mda mfupi uliopita alisema amepoteza madaraka ya kukaimu nafasi hiyo kuhamasisha amani na umoja wa vyama.
0 comments:
Post a Comment