Tuesday, November 4, 2014

HATIMAYE JENGO REFU ZAIDI LA KIBIASHARA 'WTC' LILILOTUNGULIWA NA OSAMA KUANZA KUTUMIKA TENA MAREKANI!

Jengo kubwa la biashara katika Jiji la Newyork nchini Marekani limeanza kukaribisha wapangaji wapya wa kampuni ya uchapishaji ya Conde Nast ikiwa ni miaka 13 tangu kutokea kwa shambulio la bomu lililoangusha majengo makubwa ya biashara.
TAKRIBANI watumishi mia moja sabini na tano wa uchapishaji wa majarida kama yale ya New Yorker pamoja na Vanity fair, Walijazana ndani ya jengo lilipo katika mtaa wa Vesey  hatua chache kutoka eneo la kumbukumbu na makumbusho ya jengo hilo la Twin Towers lilipokuwa hapo awali.
Jengo hilo liliangushwa baada ya kutokea shambulizi mnamo September 11 baada ya ndege za kijeshi za kigaidi za Al Qaeda kushambulia majengo hayo na kusababisha moto mkubwa pamoja na moshi kutanda.
Takribani raia elfu tatu walipoteza maisha yao,kwenye mashambulizi hayo na ambapo pia ndege hizo zililenga jengo la Pentagone.
Jengo hilo lenye thamani ya dola za Kimarekani bilioni 3.8 limechukua muda miaka nane kulijenga na kwa sasa ndilo jengo refu kuliko yote nchini Marekani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI