Kamati ya uandaaji wa michuano ya Olympic imemteua Mchezaji mstaafu wa mchezo wa kuteleza maarufu kama Scatting, Kim Yu kuwa balozi wa Heshima katika michuano ya Olympic ya majira ya baridi inayotarajia kufanyika mwaka 2018 katika mji wa Pyeongchang,huko Korea ya Kusini.
Ni manjonjo na bashasha zikioneshwa na mchezaji huyu kabla ya kutundika daruga na hapa ni katika michuano ya Olympic iliyofanyika mjini Sochi nchini Russia mapema mwaka huu ambapo aliibuka kidedea kwa kuchukua medali ya Silver .
Kim akiwa ni sehemu ya wanakamati wanaoutangaza mji wa Pyeongchang amewaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia fahari kubwa kuwa balozi wakati huu ambapo mashindano haya yatafanyika katika nchi yake na kuahidi kuwa atafanya kila linalowezekana kuhakikisha anaitangaza michuano hii ya majira ya baridi.
Kim mwenye umri wa miaka 24 alistaafu baada ya kushinda medali ya Silver katika michuano ya Olympic iliyofanyika Sochi mwaka huu pia alishinda medali ya dhahabu katika michuano ya Olympic ya 2010 iliyofanyika Vancouver katika ubingwa wa dunia 2009 na 2013.
0 comments:
Post a Comment