Tuesday, November 4, 2014

TAYLOR SWIFT AONDOA NYIMBO ZAKE KATIKA MTANDAO WA SPOTFY

Mwanamuziki maarufu wa miondoko ya country duniani Taylor Swift amewashitua mashabiki wake na tasnia nzima ya burudani duniani baada ya kuondoa albamu zake zote kwenye mtandao maarufu unaotoa huduma ya kusikiliza nyimbo Spotify.
MWANAMUZIKI huyo aliyeimba wimbo wa shake it off hivi sasa ameitingisha kampuni ya spotfy na kuwaacha midomo wazi kwa kuamuru nyimbo zake zote na albamu kutolewa siku chache baada ya kampuni hiyo spotfy kumkosoa swift kwa kutoweka albamu yake mpya 1989 katika mtandao.
Hii si mara ya kwanza kwa mwanadada huyu machachari kupinga kuwa hafikirii sana kuhusu huduma ya muziki mitandaoni kwani hata albamu yake ya mwaka 2012 iitwayo Red haikuwapo katika mtandao mpaka miezi kadhaa ilipopita tangu kuachiliwa.

Mapema mwaka huu Swift aliandika katika jarida la Op Ed For the wall street  kuwa muziki ni sanaa na sanaa ni muhimu lakini pia ni nadra na vitu nadra ni vya thamani hivyo lazima vilipiwe, Taylor swift alizungumza haya akitetea thamani ya uwepo wa muziki katika mitandao.

Ikumbukwe kuwa mwezi march mwaka huu kampuni ya Billboard ilimtaja Taylor swift kuwa ndio mwanamuziki anayelipwa hela kubwa zaidi nchini marekani kwa makadirio ya mwaka 2013 kuwa aliingiza takriban dola za kimarekani milioni 40. Swali ni je Kuondoka kwake spotfy kutampunguzia mashabiki na pesa anazoingiza au la?

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI