Tuesday, November 11, 2014

EWE SHABIKI WA UKWELI WA JOKATE HUTAKIWI KUIKOSA HII MPYA TOKA KWA JOJO KIDOTI

MWANAMITINDO, mtangazaji wa TV na msanii wa muziki na filamu Jokate Mwegelo ameingia tena ndani ya studio za Pesa Records chini ya producer Allonem na kuandaa wimbo mpya uliopo kwenye hatua za mwisho.
Akizungumza na Bongo5 hivi karibuni producer wa studio hiyo Allonem, alisema Jokate amebadilika na kuimba nyimbo za Kiswahili na kudai amebadilika kutoka kwenye uimbaji wa kutumia Kiingereza zaidi
“Jokate tumefanya naye kazi mbili, moja imeshatoka ni ile ambayo ali-perform kwenye show ya Fiesta Mwanza na baada ya hapo tukakaa chini na kuandaa wimbo mpya ambapo mpaka sasa hivi upo katika hatua za mwisho,” amesema producer huyo.
“Sema Jokate sasa hivi yuko mbio sana ila akitulia itamalizika.
Pia studio ya Pesa Record tukiwa chini ya mkurugenzi wetu Mwinyi Pesa tumeanzisha Pesa Entertainment ambayo ina msanii Becka Title. Atatoa wimbo ijumaa hii itakuwa kama ndo kama anatuzindulia licha ya kuwa kuna mambo mengine yatafuata,” aliongeza Allonem ambaye pia alitengeneza beat ya wimbo wa Fid Q na Bi Kidude.

0 comments:

Post a Comment