MSANII mkongwe wa Bongo fleva Dully Sykes amesema wimbo wake aliomshirikisha Maunda Zoro uliovuja hivi karibuni, ulirekodiwa miaka sita iliyopita kipindi ambacho alikuwa bado kwenye ‘foolish age’.
“Hiyo ni ngoma ambayo imevuja ni ya siku nyingi sana, kwasababu kwanza hata nilikuwa sijui ilipo wapi kwasababu ni nyimbo ya kuanzia Dhahabu Records, kabla hata sijafungfua studio nyingine.” Dully ameiambia Bongo5.
“Mimi nimeiacha tu ivuje kwasababu siwezi hata… nyimbo kama hiyo kweli unaweza hata kuifanyia video? Siwezi, hiyo nyimbo tangia mwaka 2008,mpaka sasa hivi karibia miaka sita.”
Baada ya wimbo huo kuvuja Dully amesema unaweza kutumika sehemu zinazoweza kuruhusu nyimbo za aina hiyo (matusi), lakini ameomba usisambazwe wala kupigwa kwenye redio.
“Inaweza kupigwa club inaweza kupigwa kwenye ma pub au sehemu yoyote sio mbaya kama itasambaa kwa njia hiyo lakini sio ivuje isambae kwa njia ya media kwa radio. Kwasababu hata miaka ambayo nimerekodi hiyo pia ilikuwa miaka ya foolish age, na sasa hivi nina miaka yangu iko tofauti kabisa miaka sita mbele ina maana hata akili yenyewe imebadilika.” Alimaliza
Isikilize ngoma hiyo hapa chini…!
0 comments:
Post a Comment