Katibu Tawala Wilaya Sengerema Bw. Focus Majumbi, (katikati) akishudia nyavu haramu kabla ya kuchomwa. Wa kwanza kushoto ni Afisa elimu msngi Wilaya Sengema Juma Mwajombe na Kulia ni Afisa uvuvi shupavu Bw. Henry Kaswahili.
Na Daniel Makaka, Sengerema
Zana haramu za kuvulia Samaki zinazokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni mia mbili na laki tani zimekamatwa na kuteketezwa na Afisa uvuvi tarafa ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza Bw.Henry Kaswahili.
Kwa mujibu wa taarifa yake katika hafla ya kisomo cha watu wazima, ambayo pia ilitumika kuchoma zana hizo haramu, zana zilizochomwa ni pamoja na Kokolo 8 za Sangara; Timba 2,525; Kokolo za dagaa 3; Mitubwi 33 iliyokuwa inajihusisha na uvuvi haramu na nyavu ndogondogo 50.
Kwa ujasiri huo, Katibu tawala wa wilaya Sengerema Bw. Focus Majumbi amempongeza Afisa huyo na kusema ni mfano wa kuigwa kwa kukamata nyavu haramu na kuziteketeza kwa moto.
Afisa uvuvi Henry Kaswahili akianda nyavu haramu ili zichomwe moto.
Akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya juma la elimu ya watu wazima Wilayani Sengerema yaliyofanyika katika kijiji cha Nyakalilo Tarafani Buchosa ambako kazi ya uchomaji wa nyavu hizo haramu ilifanyika alisema kiongozi huyu anapaswa kupongezwa kutokana na umahili wake wa kukamata zana hizo kisha kuziteketeza kwa moto.
Kwa upande wake Afisa uvuvi huyo alisema ameamua kupambana na uvuvi huo haramu kwakuwa umekithiri na umekuwa tishio wilayani Sengerema na ameahidi kuutokomeza katika maeneo anayoyaongoza akishirikiana na na raia wema.
Nao wananchi waliokuwa wamekusanyika kushuhudia uchomaji wa nyavu hizo haramu pamoja na viongozi wengine wamempatia sifa lukuki kwa kuonesha nia na njia ya kudhibiti uvuvi haramu wilayani humo.
Viongozi na wananchi wakishudia zoezi la uchomaji nyavu haramu.
Wananchi wakishudia na nyavu haramu kuteketezwa.
Chanzo: MO blog
0 comments:
Post a Comment