MECHI nne
za Kundi A la Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimefanyiwa marekebisho ili
kutoa fursa ya matumizi ya Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Timu za African
Lyon na Kimondo FC ambazo awali zilikuwa zicheze Oktoba 25 mwaka huu
kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani, sasa zitacheza Oktoba 26 mwaka
huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Nayo
mechi ya Polisi Dar es Salaam na Majimaji ya Songea iliyokuwa ichezwe
Oktoba 26 mwaka huu Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, sasa itachezwa
Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
Mechi ya Friends
Rangers na Ashanti United iliyokuwa ichezwe Mabatini mkoani Pwani,
Oktoba 26 mwaka huu, sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Oktoba 28 mwaka
huu.
Pia mechi
ya Lipuli FC na JKT Mlale iliyokuwa ichezwe Oktoba 25 mwaka huu kwenye
Uwanja wa Samora mjini Iringa, imesogezwa mbele kwa siku moja. Mechi
hiyo sasa itachezwa Oktoba 26 mwaka huu kwenye uwanja huo huo.
0 comments:
Post a Comment