Thursday, October 16, 2014

NDEGE ISIYO NA RUBANI YADONDOSHA BENDERA UWANJANI NA KUPELEKEA WACHEZAJI KUPIGANA NGUMI *PICHAZ*

KATIKA hali isiyo ya kawaida mechi kati ya Serbia na Albania imeshindwa kumalizika baada ya ndege isiyokuwa na rubani kubeba ujumbe wa kisiasa kusababisha vurugu zilizowahusisha wachezaji na mashabiki ndani ya uwanja wa Partizan.
Mechi hiyo ya kufuzu katika michuano ya soka bara la Ulaya mwaka 2016 ilisimamishwa na mwamuzi Martin Atkinson kutoka Uingereza katika dakika ya 41 ya mchezo huo huku matokeo yakisomeka 0-0.
Vurugu ziliibuka wakati bendera ya Albania na ujumbe kupeperushwa juu ya uwanja na kushikwa na wachezaji wa Serbia. Wachezaji wa Serbia walijaribu kuichukua bendera hiyo mbele ya mashabiki kadhaa ilichanika ndani ya uwanja.
'Tukio moja la kijinga limesababisha vurugu- hiyo ndio njia ya mkato kulielezea tukio lililotokea usiku' alisema mwandishi wa televisheni ya B92 Milos Saranovic.
Mwamuzi Atkinson aliwaondoa wachezaji nje ya uwanja na baada ya kuchelewa kwa dakika 30 Uefa ilithibitisha kusitishwa kwa mchezo huo.


Mechi ya Abania na Serbia yatibuka.

Serbia na Albania wana historia ya kutoelewana mara kwa mara ikihusishwa na jimbo la zamani la Serbia Kosovo jimbo ambalo lilijipatia uhuru mwaka

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI