Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing
Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing
Nakaaya Ashusha Kitu Kipya Sokoni, Ni Katika Albam Blessing
MSANII wa
muziki wa kizazi kipya Nakaaya Sumari hivi karibuni alikonga nyoyo za
mashabiki wake kwa kuzindua albam mpya iendayo kwa jina la Blessing
yenye nyimbo kumi na mbili (12).
Albam
hiyo ambayo ni albam yake ya pili ilizinduliwa jijini Arusha na
kuhudhuriwa na mashabiki wa muziki wake kutoka mikoa ya Arusha, Manyara
na Kilimanjaro. Huku akiungwa mkono na wasanii wenzake kutoka hapa hapa
nchini na nje ya nchi.
Uzinduzi
huo ulipambwa na burudani kabambe kutoka kwa Hisia, G Nako, Jambo squad
wote kutoka Arusha, Naaziz kutoka Kenya, na Nakaaya mwenyewe yote
hiyonikumpasapotimsaniimwanzao.
Akizungumza
kwa furaha mwanadada Nakaaya Sumari alisema kuwa anawashukuru sana wote
waliokuja kumuunga mkono katika uzinduzi wake.
“Nawashukuru sana
mashabiki wangu kwa kunipa sapoti ya nguvu kwani wa lijitokeza kwa
wingi, nimefurahi sana kwani huu ni mwanzo mzuri,” alisema Nakaaya.
“Albam
hii imebebwa na wimbo wa Blessing ambao ni maalum kwa mwanangu kipenzi
kwani yeye ni Baraka kwangu hata napokua mbali naye bado nakua na
matumaini na faraja,” Nakaaya aliongeza kwa msisitizo.
Albam ya
Blessing ipo sokoni sasa na inanyimbo nzuri za kuelimisha, kuburudisha
na kuliwaza kama vile Utu uzima dawa, Temana na watu, Blessing,
Beautiful, I am an African, Sister sister, Ngufurie, na Mwanamke shujaa,
kubwa ni kumpa sapoti kwa kununua albam hii
0 comments:
Post a Comment