Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akifuatilia kwa makini mkutano wa kundi namba 1 la nchi za
Afrika- Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Aliye kaa
nyuma yake ni Kamishna wa Fedha za Nje Bw. Saidi Ngosha Magonya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa serikali Dr. Servacius
Likwelile akisoma nyaraka za mkutano wa kundi namba 1 la nchi za Afrika-
Benki ya Dunia ambao umefanyika leo hapa mjini Washington DC. Picha
zote na Ingiahedi Mduma- Wizara ya Fedha.
***********
MKUTANO
wa kundi namba 1 la nchi za Afrika hufanyika kila mwaka wakati wa
mikutani ya Benki ya Dunia na IMF na unahusisha kundi la nchi za Benki
ya Dunia ambazo zinapata mikopo nafuu kutoka IDA. IDA ni shirika au
mfuko wa maendeleo kwa ajili ya kutoa mikopo nafuu kwa nchi
zinazoendelea kwa kundi la Benki ya Dunia.
Katika
mikutano hii wanazungumzia zaidi masuala ya sera za kibenki na mambo ya
utawala kama vile ajira , uchaguzi wa wenyeviti wa mikutano hiyo na
kamati mbalimbali. Mkutano huo unaudhuriwa na Mawaziri wa Fedha. Kwa
mwaka 2014 -16 Mwenyekiti atakuwa Waziri wa Fedha kutoka Ethiopia na
Makamu wake anatoka Gambia. Viongozi hawa wataongoza mpaka mwaka 2016.
Mwaziri wa Fedha ni Magavana na Matibu wakuu ni MaGavana mbadala, hivi
ni vyeo vya uwakilishi kattika Benki ya Dunia.
Akiongea
katika mkutano huo mwenyekiti aliyemaliza muda wake alisema
kuwa”tumepata Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kundi la kwanza la nchi za
Afrika ambaye anatoka visiwa vya Shelisheli na Mbadala wake anatoka
Zimbabwe “ alisema.
Akiendelea
kuzungumza katika mkutano huo aliwaambia wajumbe kuwa anayemaliza muda
wake anatoka Zambia na kuwa Viongozi hawa wanachaguliwa kwa kupigiwa
kura na kila nchi. “Hawa watakuwa watendaji moja kwa moja kuanzia sasa
na nafasi hizi zinapatikana kwa mzunguko.”alisisitiza.
Vilevile
katika kundi hilo kutakuwa na kamati ya maendeleo ambayo itakuwa na
mwenyekiti ambaye atatoka Uganda na wajumbe watatoka Tanzania, Namibia
pamoja na Sierralion.
Jambo
lingune ambalo limeongelewa kwenye mkutano huo muhimu ni kwamba Benki
itaendelea kutoa misaada ya fedha kwa nchi zinazoendelea toka kwenye
mfuko wa IDA kwa kuzingatia vipaumbele vya nchi husika.
Vilevile
walisisistiza suala la gonjwa la EBOLA. Walielezea kuwa wataendelea
kusaidia kupeleka misaada kwa nchi zinazokabiliwa na hilo tatizo. Pia
Benki ya Dunia itaendelea kupeleka wafanyakazi kujifunza jinsi Benki ya
Dunia inavyofanya kazi na kusisitiza kuwa ni muhimu kuchagua watu wazuri
ambao wana uwezo ili wanaporudi nchini kwao waweze kutumia ujuzi wanao
upata.
Mwisho
walimalizia kwa kusema kuwa Benki itaendelea kusaidia jitihada ambazo
zinalenga matokeo makubwa sasa kwani hata wao wanafanya kazi kwa
kuzingatia matwakwa ya BRN. Hivyo wanatagemea fedha zinazotolewa
zitafanikisha kuwa na matokeo makubwa sasa. Hali ya hewa mjini hapa ni
baridi kiasi.
0 comments:
Post a Comment