Pichani
(wa tatu kulia),Meneja Matekelezo Mfuko wa Pensheni wa LAPF,Bwa.Victor
Kikoti akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani), mapema leo
katika ofisi zao zilizopo jengo la Millenium Tower,Kijitonyama jijini
Dar,kuhusiana na kufanyika kwa mkutano wao wa 7 wa mwaka wa wadau
kuanzia Oktoba 23 mpaka 24, 2014.
**********
MKUTANO
huo utafanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano (AICC),jijini
Arusha.Bwa.Victor amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni ''
kusherehekea miaka 70 ya ukuaji na huduma bora kwa Wanachama''. '' Kauli
mbiu hii imefikiwa baada ya mfuko kutimiza miaka 70 tangu ulipoanzishwa
mwaka 1944,ambapo Wadau wa mkutano huo watajadili kwa kina juu ya
huduma za LAPF kwa miaka 70iliyopita pamoja na kushiriki mafanikio ya
mfuko kwa pamoja.
Matekelezo
Mfuko wa Pensheniwa LAPF,Bwa.Victor Kikoti amesema kuwa,Mgeni rasmi
katika mkutano huo anatarajiwa kuwaWAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh.Hawa Ghasia
Pichani
kulia ni Meneja Mkoa Bwa.Ramadhani Mkeyange,Meneja Takwimu,Tathmini na
Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata pamoja na Meneja wa Kanda ya Dar,Bi.Amina
Kassim
Meneja
Takwimu,Tathmini na Hadhari Bwa.Abubakar Ndwata,akifafanua moja ya
swali aliloulizwa na Waandishi wa Habari kuwa mfuko wa LAPF unaendelea
kujivunia mafanikio ya kuwa mfuko unaokuwa kwa kasi hapa nchini pamoja
na kuwa bora kwa miaka mitano mfululi kwenye suala zima la uwajibikaji
na utunzaji wa vitabu.
Amesema
kuwa mfuko pia utazindua logo mpya inayotumika,ambayo inaashiria
ukuaji wa mfuko huo na dhamira yao ya kuendelea kukua zaidi na
kuboresha huduma kwa wanachama wao,ameongeza kusema kuwa mfuko huo
utatoa fursa mpya ya mkopo wa elimu kwa wanachama wake ilivyozinduliwa
mwezi Agosti mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment