ALICIA KEYS ameonesha kuguswa na tukio zima la utekaji wa wasichana wa Chibok wanaotimiza miezi sita sasa tangu wawe katika mikono ya Boko Haram huko katika jimbo la Borno tangu April 14.
Msanii huyo amechukua jukumu la kuwaongoza kinamama na kuandamana nao mpaka makao makuu ya Umoja wa mataifa huko New York, nchini Marekani wakiomba nguvu zaidi ziongezwe ili waachiliwe huru.
Alicia Keys amesema kuwa ni vyema jambo hili likaongelewa sana hadi waachiliwe kwani binadamu wanahulka ya kusahau na kuendelea na maisha yao..!
0 comments:
Post a Comment