Mwanadada Daniela
aliishi na mdudu huyo kwenye pua lake kwa mwezi mmoja
MWANAMKE mmoja aliyekuwa
amesafiri kwenda Kusini mwa Bara Asia, alishtuka alipogundua kuwa mdudu
anayeitwa Kaka au 'Leech' kwa kimombo na ambaye hunyonya damu alikuwa anaishi
katika pua lake.
Mdudu huyo alikuwa na urefu wa nchi 3.
Mwanadada huyo aligundua uwepo wa mdudu huyo katika pua lake baada ya kurejea
kutoka katika safari yake ya bara Asia.
Daniela Liverani, mwenye umri wa miaka
24, kutoka mjini Edinburgh, Scotland, amekuwa akivuja damu kutoka katika pua
lake kwa wiki kadhaa.
Hata hivyo alidhani labda mshipa mdogo
wa pua lake ulikuwa umepasuka baada ya kupata ajali akiwa anaendesha pikipiki.
Bi Liverani alikuwa bafuni wiki jana
Alhamisi alipogunduya mdudu huyo kwenye pua lake alipoona kitu kikionekana
kikisonga songa katika pua lake.
Wahudumu wa hospitali, walitumia vifaa
vidogo kumuondoa mdudu huyo kutoka katika pua la Daniela.
Bi Liverani anaamini kuwa mdudu huyo
aliingia katika pua lake alipokuwa safarini Vietnam au Cambodia lakini hata
alipohisi kitu kikitembea kwenye pua lake alidhani labda ilikuwa damu iliyokuwa
imeganda.
''Mimi nilidhani tu ilikuwa damu
iliyokuwa imeganda,kwenye pua langu,'' alisema Daniela.
Wakati Bi Liverani alipoingia bafuni
ndipo mdudu huyo alioenakana kwa haraka kwa sababu ya mvuke uliotokana na maji
moto ambayo yaliwezesha mdudu huyo kuteleza.
Hata hivyo alipogundua mdudu huyo
alikwenda hadi hospitalini ambako mdudu huyo alitolewa kwenye pua la mwanadada
huyo.
''Madaktari walifanya kazi nzuri sana,
ninawapongeza, kwa sababu sio kawaida kwao kuona kitu kama hiki kila siku,''
alisema Liverani.
Chanzo: BBC Swahili
0 comments:
Post a Comment