Thursday, October 9, 2014

GREEN WASTE PRO LTD YAKABIDHI MAKASHA YA KUHIFADHIA TAKA SHULE YA MSINGI BUNGE

DSC_0062
Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena akikabidhi rasmi moja kati ya makasha matatu ya kuhifadhia taka yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Mwalimu wa klabu ya mazingira wa shule ya msingi Bunge, Mwl. Frida Madanganya. Kulia ni Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
DSC_0003
Baadhi ya michoro iliyopo kwenye majengo ya shule ya msingi Bunge yanayohamasisha utunzaji wa mazingira kwa wanafunzi wa shule hiyo.
DSC_0102
Wanafunzi wa klabu ya mazingira shule ya msingi Bunge wakiagana na Meneja wa uendeshaji wa kampuni ya  Green Waste Pro Ltd, Abdallah Mbena aliyeambatana na Afisa Rasilimali watu wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Naima Mpili.
 **********
Na Mwandishi wetu
KAMPUNI ya Usafi ya Green Waste Pro imetimiza ahadi yake ya kuipatia shule ya Msingi Bunge makasha ya kuhifadhia taka na vifaa vya usafi wa mazingira  iliyoitoa mwaka jana.

Mwaka jana wakati wanafanya shughuli ya kupaka rangi shule hiyo,kampuni hiyo ilifurahishwa na mazingira ya shule jinsi yanavyotunzwa kiasi cha kufanya maamuzi ya kuwapelekea vifaa vya mazingira na hasa makasha ya kuhifadhia taka.

Kwa mujibu wa Afisa uendeshaji wa kampuni hiyo Abdallah Mbena,ambaye ndiye aliyekabidhi makasha hayo,maamuzi ya kuwapatia makasha yametokana na jinsi klabu ya mazingira  ya shule hiyo na mwalimu wao anavyochakarika katika kuhakikisha usafi wa mazingira katika shule hiyo.

Mbena alisema kwamba wamefarijika sana na juhudi zinazofanywa na mwalimu na wanafunzi wake katika kuhakikisha kwamba wanatunza mazingira.

Pamoja na sababu za wanafunzi hao na mwalimu wao katika kutoa kipaumbele mazingira, kuwa chanzo cha kutolewa kwa makasha hayo, sababu nyingine iliyozingatiwa ni kuwa shule hiyo ipo katika kata ya Kivukoni ambapo kampuni hiyo inazabuni ya kufanya usafi.

Amesema wana mpango wa kuwapatia vifaa vya aina hiyo kwa shule nyingine zinazofanya vyema kwenye usafi wa mazingira ila kwa sasa wameanza na shule ya Bunge.

Mwalimu wa mazingira wa shule hiyo, Frida Madanganya ameshukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kuwasaidia na anawategemea wataendelea zaidi kuhakikisha kwamba shule hiyo inakuwa namba moja kwa utunzaji wa mazingira.

Naye Mwalimu Mkuu Khadija Telela alisema shule yake ina changamoto kubwa hasa maji ya Dawasco kwani maji yao ni yachumvi kwa kisima walichochimba.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI