Friday, September 19, 2014

LINAH AANGUKIA KATIKA FILAMU, ASHIRIKI KATIKA FILAMU NA LULU

Tumeshashuhudia baadhi ya waigizaji wa Bongo Movie ambao wamejaribu bahati zao upande mwingine wa sanaa kwa kujitosa kwenye muziki kama Shilole, na pia baadhi ya wasanii wa muziki kuamua kujitosa kwenye Bongo Movie.
Mwimbaji wa R&B Linah Sanga ameingia kwenye orodha ya wasanii wa muziki ambaowameanza kujihusisha na filamu, ambaye anatarajia kuonekana kwenye filamu mpya aliyocheza na Lulu.
MUIGIZAJI wa kike wa Bongo Movie ambaye alianza kuigiza akiwa na umri mdogo Elizabeth Michael aka Lulu anatarajia kuachia filamu mpya inayoitwa ‘Mapenzi Ya Mungu’, ambayo amecheza Linah.
Linah ameiambia Bongo 5 jinsi alivyopata nafasi ya kushiriki kwenye filamu hiyo ambayo ndio filamu yake ya kwanza kushiriki.
“Kipindi kile alichokuwa ametoka (Lulu), ametoka kama ana wiki mbili akanipigia simu akaniambia kuna movie nafanya na movie yenyewe nafikiri unaweza ukafanania na hiyo movie kulingana na kitu ambacho tumekiigiza humo ndani mambo mambo ya gospel imekaa kimambo mambo flani ya kidini dini kwa mbali kiaina”. Alisema Linah. 

“Kwa hiyo akaniambia nafikiri utafaa nilikuwa natamani siku moja mije nifanye movie na wewe sababu nakupenda nakukubali hivyo,hamna mtu yeyote alinishawishi kwahiyo nikajaribu kuongea na viongozi wangu wakaniambia ts fine fanya kama unaweza, kwahiyo hiyo ndo movie yangu ya kwanza kufanya kama Bongo movie na sijui aliniamini vipi kama ntaweza kucheza, nashukuru nimeweza kufanya vile ambavyo yeye alikuwa anataka”.
Linah pia alielezea nafasi aliyoshiriki katika filamu hiyo.
“Mle kama naweza nikasema sio supporting character kwasababu na mimi nimekuwa kama main character kwasababu nimecheza movie nzima mwanzo mpaka mwisho, kwahiyo naweza nikasema na mimi movie imenihusu kwa upande flani, kama main character tulikuwa wawili mimi naye, tumecheza almost movie nzima kwenye kila scene nilikuwepo ni scene chache sana naweza nikasema labda nne tatu ambazo sikuwepo”.
Mwimbaji huyo wa ‘Ole Themba’ amesema mapokeo ya filamu hiyo itakapotoka ndio yatampa picha kama aanze kujihusisha kwenye filamu zaidi au laa.

“Kwa experience ambayo nimepata kwenye movie ya Lulu nina uhakika najinaweza nikacheza movie yoyote”.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI