Friday, September 26, 2014

ALI KIBA VS DIAMOND: ALI KIBA ANAPENDWA UINGEREZA KULIKO DIAMOND…. FAHAMU UKWELI HAPA!!!

MABISHANO ya mashabiki kuhusu ni nani mkali kati ya Diamond na Ali Kiba ulionekana kufifia kwa muda kidogo kwenye media lakini ukweli ni kwamba pressure iliyoko mitaani kiuhalisia kwa wasanii hawa inafanya mada hiyo kutoepukika kirahisi.
Mtandao wa Bongo5 umeibua gumzo jingine baada ya kufanya mahojiano na promota wa muziki na filamu anaefanya kazi zake nchini Uingereza, Hadija Seif, maarufu kama Dida Fashion na alisema nchini humo Ali Kiba anapendwa zaidi ya Diamond.
“Sio sasa hivi tu, tangu zamani to be honest kwa UK Alikiba yupo juu zaidi.  Sijui kwanini lakini kwa watu wenyewe ukisema labda kati ya Ali kiba na Diamond hapo nani aletwe, honestly watu wa UK yaani Ali kiba sijui aliwafanya nini lakini Alikiba UK is the best.” Alisema promota huyo.
Hata hivyo, ripoti hiyo ilipokelewa kwa hisia tofauti mashabiki wa muziki.
Mtu mmoja anaetumia jina la Blacksailors Jangombwe kwenye Facebook, yeye ni mtanzania anaeishi Uingereza ambaye alitofautiana na ripoti ya Dida.
Hiki ndicho alichoandika:
“Please Dida Please!!. If you can’t afford to hire someone, doesn’t mean he’s not popular then the one you just mention. kuwa mkweli uliweza kumleta diamond UK before but now you can’t,because he’s very expensive. Sasa unaposema UK wanampenda fulani then fulani kwaushahidi upi??. have u done a survey If YES when and which county in UK. Watu wamejaa kwenye holli waiting up to 5:00 am. Unafikiri angekua huyo unaemtaja wewe, Nani UK ungemueka asubiri mpaka saa 11 alfajiri Common Dida. Msema ukweli ni mpenzi wa mungu. Better to try another way to promote DIDA ENT. Northampton peoples know better than thaaaaaaat!!!!. Common sister you know we always love you and support you,don’t do that, TheTruth is matter.”

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI