Friday, September 26, 2014

"JAMANI SASA NAFAA KUWA MKE NIMESHAMALIZA UJANA" - WOLPER AFUNGUKA *PICHAZ*

Staa mkali wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper.
*****
STAA mkali wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper amefunguka kuwa kwa sasa yuko tayari kuolewa kwani anaamini anastahili kuwa mke.
Wolper alisema, katika maisha siku zote anaamini kuna kipindi kinapita cha kufanya ujana ambacho tayari ameshakipitia na sasa ni muda wa yeye kutengeneza familia.
“Naamini kabisa huu sasa ni muda muafaka kwangu, niko tayari kabisa kuwa mke maana nimepitia vitu vingi ambavyo mara nyingi wengi wao huwa wanakimbilia kwenye ndoa wakiwa bado hawajavimaliza halafu mwisho wa siku wanazishindwa, mimi nishamaliza vyote,” 
alisema Wolper pasipo kufafanua kama tayari ameshampata mchumba au la.
Jacqueline Wolper akipozi.
Wolper amewahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na  mastaa kadhaa akiwemo Mohamed Mtoro ‘Dalas’ ambaye alimbadilisha dini ili waweze kufunga ndoa lakini ikaota mbawa.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI