Thursday, August 7, 2014

SHINYANGA KESHO HAPAKALIKI,MPANGO MZIMA NI KATIKA UWANJA WA KAMBARAGE KUANZIA SAA 2 ASUBUHI, MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI KUTIMUA VUMBI

Picha ikimwonesha mwanamke akiwa katika mashindano ya mbio za baiskeli huku akiwa amebeba ndoo ya maji kichwani.Kesho katika uwanja wa ccm Kambarage mjini Shinyanga katika kusherehekea sikukuu ya Nane nane mbio za namna hiyo zitakuwepo.

MASHINDANO ya mbio za baiskeli kwa kanda ya ziwa na mashariki yanayojulikana kama (safari lager bike race 2014) yanatarajiwa kufanyika kesho  Ijumaa mjini Shinyanga  kwa ikiwa ni ngazi ya mkoa katika uwanja wa CCM Kambarage wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima nchini (Nane Nane).
Kwa mujibu wa meneja mauzo wa TBL kanda ya magharibi  Robert Kazinza lengo kuu la mashindano hayo ni kujenga uhusiano wa kimichezo kupitia mchezo wa Baiskeli,kupromote bia safari lager kupitia kampuni ya TBL,kutoa burudani,kusapoti sera ya serikali ya kuinua michezo.
Amesema mashindano hayo katika miaka yote yamekuwa yakidhaminiwa na TBL kupitia bia yake ya Safar Lager na kwa ngazi ya mkoa mwaka huu yanafanyika mkoani Shinyanga na kikanda yatafanyika jijini Mwanza.
Kazinza amesema lengo la kampuni ya TBL kupitia bia ya safari lager kudhamini mashindano hayo ni kufufua mitaji ya wajasiliamali kanda ya ziwa kwa kuwa michezo ni ajira.
Tayari washiriki wameshawasili tayari mjini Shinyanga kwa ajili ya mashindano hayo kuanzia saa moja asubuhi ambapo mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.  
Amesema zawadi za mashindano hayo kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume(Mbio za baiskeli kutoka uwanja wa Kambarage-Kahama/Kahama-Shinyanga) ambapo ni sawa na kilomita 250 ataondoka na kitita cha shilingi milioni moja, mshindi wa pili shilingi laki nane na mshindi wa tatu atajinyakulia shilingi laki sita,mshindi wa nne laki 5,mshindi wa tano laki 3,mshindi wa 6 hadi kumi ataondoka na shilingi laki moja,na mshindi wa 11 hadi 20 watapata shilingi elfu 50.
Kazinza ameongeza kuwa mshindi wa kwanza kwa mbio za wanawake kilomita 150(Shinyanga-Isaka/Isaka-Shinyanga) atajizolea kiasi cha shilingi laki saba, mshindi wa pili laki tano na mshindi wa tatu atajibebea kiasi cha shilingi laki tatu, wa laki 2, wa tano laki moja na nusu,wa sita hado wa 10 ataondoka na shilingi laki ,  na mshindi wa 11 hadi 20 ataondoka na shilingi elfu 50 kila mmoja.
Pia kutakuwepo mbio za watu wenye ulemavu pamoja mbio za akinamama wakiwa wamebeba ndoo za maji kichwani kuzunguka uwanja wa Kambarage ambapo washindi wote watapatiwa zawadi nono.
Katika kunogesha sikukuu ya wakulima pia kutakuwepo na ngoma za asili na shamra shamra zitaanza saa mbili asubuhi katika uwanja wa Kambarage.
Mashindano ya mbio za baiskeli kwa kanda ya ziwa na mashariki yanayojulikana kama (safari lager bike race 2014) yalianza rasmi mwaka 1998, na yalianzia mkoani Mwanza na mwaka huu ni awamu ya 16 tangu kuanza kwake.
Na Malunde Blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI