Saturday, August 23, 2014

JKT YABADILISHA TAREHE YA KUJIUNGA NA JESHI HILO SEPTEMBA 2014

TANGAZO
JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) LINAWATANGAZIA VIJANA WOTE WANAOTAKIWA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWEZI SEPTEMBA KUWA WANATAKIWA KURIPOTI VIKOSINI TAREHE 13 SEPTEMBA 2014 BADALA YA TAREHE 04 SEPTEMBA 2014.
VIJANA WANAOTAKIWA KURIPOTI  NI KAMA IFUATAVYO:-

1. WALIMU WOTE NGAZI YA CHETI (GATCE) 2014. (WALIOMALIZA 2014).

2. WALIMU ELFU TATU NGAZI YA DIPLOMA (DSEE) (WALIOMALIZA 2014).

3. VIJANA WA KIDATO CHA SITA AMBAO HAWAJAANDIKA BARUA ZA KUOMBA KUAHIRISHA KAMA ILIVYOTOLEWA MAELEKEZO YA AWALI.
AIDHA JKT LINAKANUSHA UVUMI UNAOENEZWA KWA NJIA YA UJUMBE MFUPI WA MANENO "SMS" NA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII KUWA VIJANA WA KIDATO CHA SITA WANAOENDA VYUO VIKUU  WANATAKIWA KWANZA KWENDA KWENYE MAKAMBI YA JESHI KUCHUKUA BARUA ZA KURUHUSIWA KWENDA VYUONI, TAARIFA HIZI SI ZA KWELI BALI NI UZUSHI NA UPOTOSHAJI.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA  NA MAKAO MAKUU YA JESHI LA KUJENGA TAIFA.
Chanzo: JKT

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI