Wednesday, August 6, 2014

GOTI LACHELEWESHA USAJILI WA VIDAL MANCHESTER UNITED

Future doubt:  Arturo Vidal's move to Manchester United and Juventus could still go ahead
USAJILI wa kiungo Arturo Vidal kutoka Juventus kwenda Manchester United umepata ganzi kufuatia mashaka ya kutokuwa fiti kwa nyota huyo wa Chile, hii ni kwa mujibu wa kocha wake wa timu ya taifa.Kocha wa Chile Jorge Sampaoli ameliambia gazeti la El Mercurio la nchini humo kuwa bosi wa United, Louis van Gaal anahofia kutumia pauni milioni 47 kwa Arturo Vidal ambaye aliandamwa na maumivu ya goti.
Vidal amekuwa akiwindwa na United na kwa muda mrefu ambapo katika muda wote wa dirisha la usajili la kiangazi, usajili wake wa kwenda Old Trafford umekuwa ukionekana uko jirani.
“Najua tatizo kubwa la usajili wake wa pauni milioni 47 kwenda Manchester United ni Van Gaal kuwa na mashaka na maendeleo ya goti la Vidal,” alisema kocha Jorge Sampaoli.
Kocha huyo wa Chile raia wa Argentina, alisema ana uhakika Vidal alionyesha kiwango cha asilimia 30 au 40 tu katika michuano ya kombe la dunia kulinganisha na ubora wake uliozoeleka Juventus.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI