Dar es
Salaam.
MWENYEKITI wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji
Joseph Warioba amesema kuendelea vikao vya Bunge Maalumu la Katiba bila
kuwapo maridhiano baina ya pande zinazovutana na upande mmoja ukibaki
nje ya Bunge, ni sawa na kutumia vibaya fedha za Watanzania.
Amesema kauli
kwamba akidi ya wajumbe wa Bunge hilo imetimia na vikao vinaweza
kuendelea haiwezi kuzaa Katiba itakayokubaliwa na wananchi wote na ni
tofauti na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inavyoeleza katika sehemu ya
kufanya uamuzi.
Akizungumza
katika mahojiano na mwandishi wetu ofisini kwake Dar es Salaam jana,
Jaji Warioba alisema, "Kama uwezekano wa kukutana upo, kwa nini Bunge
liendelee kutumia fedha wakati mnajua kuwa mwisho hamtafikia uamuzi?
Jambo la msingi ni kujitahidi kuafikiana na Bunge liwe na wajumbe wote."
Kauli ya
Warioba imeungwa mkono na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba wakati
akichangia hoja ya mabadiliko ya kanuni ya Bunge hilo kwa kulitaka bunge
hilo kujitathimini iwapo baada ya mjadala litaweza kufikia uamuzi, ili
kuepuka matumizi mabaya ya fedha za walipakodi.
Akitoa
hadhari hiyo bungeni jana, Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Iramba
Magharibi na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, alisema ni vyema Bunge hilo
likajiridhisha kuhusu namna linavyoweza kutumia siku 60 zilizowekwa kwa
uhakika na umuhimu wa kuziondoa siku za Jumamosi kitendo
kinachosababisha kuongezeka hadi kufikia 84.
"Tujiridhishe
na kukubali ukweli kwamba kukaa hapa kwa siku 84 bila uhakika wa
kupatikana kwa theluthi mbili kwa pande zote mbili inayohitajika
kupitisha rasimu hii haiwezi kueleweka kwa Watanzania. Ni lazima
Watanzania watatuuliza tumefanya nini," alisema.
Alisema
kwa namna moja, ni vyema kujua idadi halisi ya wale wanaoshiriki katika
awamu ya pili ya Bunge hilo na wale wasioshiriki, ili kutoa uthibitisho
wa kihesabu kwamba uamuzi wa kuendelea kwa bunge unaweza kuwa na maana.
Hata
hivyo, Nchemba alisema ni vyema wakiendelea kujadili masuala muhimu na
kwa kuwa wanakwenda kujadili sura muhimu zinazogusa moja kwa moja maisha
ya Watanzania, lakini kwa uhakika kwamba hatua hiyo itakuwa na manufaa
kwa Watanzania katika hatua ya mwisho.
Alisisitiza
kwamba iwapo hatua hiyo itashindikana, utetezi wa mwisho hautaweza
kueleweka kwa sababu suala la kutimia kwa akidi kwa mujibu wa Katiba ni
muhimu katika kufikia uamuzi na hasa kuangalia upya umuhimu wa kufikia
maridhiano kwa sasa.
Bunge la
Katiba lilianza jana mjini Dodoma bila kuwapo kwa wajumbe wanaounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na baadhi ya wajumbe 201 wa
kuteuliwa na Rais waliosusa vikao hivyo.
Ukawa
wanashinikiza kujadiliwa kwa rasimu ya Katiba iliyotolewa na iliyokuwa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba na si ile iliyodai inaingizwa kinyemela na
wajumbe wanaounga msimamo wa CCM wa serikali mbili badala ya tatu
zilizopendekezwa na rasimu.
Licha ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kuitisha kikao
cha mashauriano kati yake, CCM na Ukawa, mwafaka haukupatikana.
Akizungumzia
hali hiyo Jaji Warioba alisema: "Hatuwezi kupata Katiba ambayo
itakubaliwa na Watanzania bila makundi yote kukubaliana. Ushauri wangu
kwa makundi yanayovutana ni kufikia mwafaka na kwenda bungeni kufanya
kazi kwa pamoja."
Alisema
kitendo cha upande mmoja kuendelea na vikao vya Bunge hilo bila upande
mwingine kuwapo, hakina faida yoyote kwa sababu mwishoni hawataweza
kuchukua uamuzi wowote.
"Hawawezi
kufanya uamuzi wowote kwa sababu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
inaeleza kuwa ili uamuzi ufanyike ni lazima iwepo theluthi mbili ya
wajumbe kutoka kila upande wa muungano.
"Itakuwa na matatizo zaidi kama mkitunga Katiba na kuipitisha kwa idadi fulani ya watu na kuanza kupingwa wakati huohuo."
Afafanua madai ya Lukuvi
Katika
hatua nyingine, Jaji Joseph Warioba alifafanua madai yaliyotolewa na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William
Lukuvi kuwa yeye (Warioba) amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha
yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Alisema
maoni hayo aliyoyawasilisha serikalini Machi 27, mwaka huu yalikuwa
maoni yaliyotolewa na wananchi lakini hayakuingizwa katika Rasimu kwa
kuwa yanahusu tu Tanganyika, kwa kuwa Rasimu iliyoandaliwa ilipendekeza
serikali tatu na Zanzibar wana utaratibu wao.
"Tuliona
kuwa sura hizo hazifai kuwa katika Katiba ya Jamhuri kwa sababu masuala
hayo mawili; ardhi, Zanzibar wana sheria na utaratibu wao, Tanzania Bara
wana sheria na utaratibu wake" alisema kama ilivyo wa Serikali za Mitaa
0 comments:
Post a Comment