Tuesday, July 22, 2014

OLE WAKO UKUTWE NA SARE ZA JESHI

KUTOKANA na kuzidi kushamiri kwa matukio ya uhalifu nchini, huku wahusika wakionekana kutumia sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), jeshi hilo limeonya na kupiga marufuku wanaovaa sare za majeshi na kutumia vifaa vyao.
Taarifa iliyosambazwa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya JWTZ kwa vyombo vya habari, inaeleza kuwa hivi karibuni kumekithiri kwa vitendo vya uovu huku wahusika wakiwa wameonekana wamevaa sare na kutumia vifaa vya jeshi hilo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI