Friday, July 18, 2014

HII NAYO KALI: NI YULE ALIYETUMIA JASHO, MACHOZI NA NYWELE KUTENGENEZA PAFYUMU!

WAKATI watu tukichukia jasho kwenye miili yetu na kutumia gharama kwa kununua marashi ya bei mbaya huku wanawake wengine wakipendelea kunukia marashi yaliyotengenezwa kwa roses, al-udi n.k msanii na mwanamitindo Martynka Wawrzyniak ameamua kufanya kitu tofauti… 
Mwanadada huyu ametumia jasho, machozi na nywele zake kutengeneza pafyumu yake aliyoiita Eau de M..
Jasho lake lilipatikana baada ya kulala na T-shirt moja kwa kwa usiku wa siku 5 mfululizo hivyo kutumia njia maalum kupata jasho lake, kupata chupa yenye machozi yake ilibidi aangalie filamu na katuni zilizomkumbusha utotoni huko nchini Poland.
Baadhi ya wanawake walitumia pafyumu yake wametoa maoni wengine wamesema inanukia kama jasho la juani huku wengine wakisemainanukia kama T-shirt ya msichana ambaye ametumia deodorant lakini haikumaliza vizuri harufu ya jasho!!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI