Sunday, June 1, 2014

ZITTO KABWE AFIWA NA MAMA YAKE


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Tanzania, (CHAWATA), Shida Salum, mama mzazi wa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA amefariki Dunia.
Kwa mujibu wa Zitto kabwe amesema mama yake alikuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Ami, Masaki, Dar es Salaam akisumbuliwa na maradhi ya saratani.

Rais Kikwete akimjulia hali mama Zitto Kabwe.
Rais Kikwete alienda kumjulia hali mama Zitto Kabwe.
Aidha bi. Shida alianza kusumbuliwa na maradhi ya saratani mapema Agosti mwaka jana lakini hali yake ilibadilika mapema mwaka huu.
Tangu kuanza kwa Bunge la Bajeti, Zitto alionekana Dodoma mara moja tu, siku ilipowasilishwa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),baadae aliondoka kwenda kumuuguza mama yake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI