Tuesday, June 17, 2014

TV 1 YADHAMINI SHINDANO LA GAME CHANGERS, MSHINDI KUPEWA MILIONI 33, SOMA HAPA!!!

KATIKA kuhakikisha kuwa watoto wa Tanzania na Afrika kwa ujumla wanapata huduma stahiki kutoka kwa jamii inayowazunguka, kampuni ya MTG kupitia runinga yake ya Tv 1 Tanzania wakishirikiana na Reach for Change Tanzania, wamekuwa ni miongoni mwa wafadhili wa shindano la kuwasaka watu wenye ujuzi na mbinu mbalimbali za kijasiriamali zinazoweza kuwakwamua watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Tanzania.
Kupitia shindano linalojulikana kama GAME CHANGER ambalo litawahusisha wale wote wenye mawazo mazuri ya kijasiriamali na moyo wa kujitolea  kwa kurudisha kile kidogo walichopata kwa jamii yao, hasa katika kuwasaidia watoto walio katika mazingira magumu na wenye kuhitaji mahitaji maalumu.
Katika mchakato huo TV 1 inawakaribisha wadau mbalimbali wanaojihusisha na kutoa huduma mbalimbali katika jamii ili waweze kuchukua fomu kwaajili ya kujiunga na shindano hilo litakalo tafuta washindi watano ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa kiasi cha dola za kimarekani 20,000 sawa na milion 33 za kitanzania, na washindi wengine wanne watapokea kiasi cha dola za kimarekani 1500 sawa na mil 2  kila mmoja.
Washindi wane waliobaki watajumuishwa pia katika mchakato huo kwa mwaka mzima na wataendelea kupewa mafunzo na uwezo wa kufanya mambo mengi ya kijasiriamali na kuwainua katika mawazo watakayoyaleta.
Hakika hili limekuja katika muda muafaka, ambapo watoto wengi nchini Tanzania watafikiwa ikiwa ni katika kuhakikisha kila mtoto anaishi katika mazingira mazuri, na hapa Mercedes Martin ambaye ni COO wa TV 1 anasema;
''TV 1 inaendelea kuthamini maendeleo ya jamii yake kwa mapana zaidi, sio tu kwa kuwaletea watanzania runinga inayotoa burudani nzuri bila kulipiwa kupitia Star Times na kuleta mapinduzi ya uzalishaji wa vipindi, bali pia kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili waweze kufanikiwa''.
Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Reach for Change nchini Tanzania na Rwanda, Richard Gorvett, akizungumza na Waandishi wa Habari.

''Tumefurahi kupata nafasi hii kupitia TV 1 ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuinua maisha ya watoto wa Tanzania. Tunaamini njia nzuri ya kuleta mabadiliko yatakayodumu katika jamii inayowazunguka ni kwa kuwasaidia wale watu wenye uchu wa kuleta mabadiliko walio na mtazamo wa kijasiriamali''. Alisema Richard Gorvett mkurugenzi wa Reach for Change Tanzania na Rwanda.
Uchukuaji wa fomu na udaili umefunguliwa rasmi na unategemewa kufungwa mnamo tarehe 07/07/2014, ambapo kwa maelezo zaidi juu ya shindano hili unaweza tembelea katika tovuti ya TV1 Game Changer na page yao ya facebook https://www.facebook.com/r4ctanzania

Changamkia fursa mdau!!!

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI