Simba
dume amejikuta katika hali tata baada ya kutolewa mkuku na Nyati katika
Hifadhi ya Kruger, nchini Afrika Kusini, walipomfumania akiwa katika
mawindo yake.
Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti.
Hakika
waswahili husema mbio za sakafuni huishia ukutani na za mwizi ni 40
siku yako ikifika hata uwe mtemi vipi watakukamata tu.
Simba akitimua
mbio huku akifuatwa kwa kasi na Nyati.
Nyati walimfikia na kumchota mtama wa aina yake na kukaa chini.
Simba alianza kula nyingi tu za uso kama alivyonaswa na camera ya Lyle Gregg.
Walipiga kila kona ya mwili wa Simba na kumjeruhi vibaya sehemu za kichwa.
Simba alipoteza kabisa ubabe wake maana mateke ya kichwa yalimuandama na pembe.
0 comments:
Post a Comment