Saturday, June 28, 2014

MTEMVU AKAGUA MADHARA YA MOTO SOKO LA KEKO, ATOA POLE KWA WAATHIRIKA

 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiingia eneo lililopata madhara kutokana na kuungua moto usiku wa kuamkia leo, katika soko la Keko, katika jimbo hilo jijini Dar es Salaam. Mtemvu amewapa pole walipoteza mali zao kutokana na moto huo ambao chanzo cha ke hakijajulikana.  Hadi inakisiwa imepatikana hasara ya zaidi ya sh. milioni 97.
 Naibu Katibu wa soko la Keko, Hassan Gitigi (kushoto) akimpa maelezo Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu kuhusu madhara yaliyosababishwa na moto huo
 Baadhi ya wafanyabiashara katrika soko hilo akieleza hasara walizopata. Wameeleza kwamba mbali na waliopata hasara ya kuunguliwa bidhaa na mabanda yaop ya biashara, pia wapo waliopata hasara kwa maduka na mabanda yaop ya biashara kuporwa na vibaka wakati wa tukio hilo la moto.
 Mtemvu akizungumza na waliopatwa na madhara kuhtokana na moto huo
Mtemvu akizungumza na baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa walipatwa na madhara kwenye soko hilo. 
Picha zote na Bashir Nkoromo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI