Saturday, June 28, 2014

HATUA YA MTOANO 16 BORA KOMBE LA DUNIA, WACHEZAJI WENYE MAJINA YA HERUFI M WENGI ZAIDI

1:- JUNI 28,  MJINI BELO HORIZOTE
BRAZIL v/s CHILE
Mshindi kati ya Brazil na Chile, atacheza na Msindi wa kati ya Colombia na Uruguay

2:- JUNI 28, MJINI RIO DE JENEIRO
COLOMBIA v/s URUGUAY
***************
3:- JUNI 30, MJINI BRASILIA 
UFARANSA v/s NIGERIA

4:- JUNI 30, MJINI  PORTO ALEGRE
UJERUMANI v/s MSHINDI WA KUNDI H
****************
5:- JUNI 29 MJINI FORTALEZA
UHOLANZA v/s MEXICO
Mshindi kati ya Uholanza na Mexico, atacheza na mshindi kati ya Costarica na Ugiriki

JUNI 29 MJINI RECIFE
COSTA RICA v/s UGIRIKI

JULAI 1 MJINI SAO PAULO
ARGENTINA v/S SWITZERLAND

JULAI 1 
MSHINDI WA KUNDI H v/S MAREKANI
Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Mashindano ya soka kombe la dunia yanaendelea kunoga na kupamba moto nchini Brazil yakijumuisha jumla ya wachezaji 892 wanaoshiriki mashindano wa mpira wa miguu duniani maarufu “Fifa World Cup” ya mwaka 2014.
Mashindano hayo yamepambwa na majina ya wachezaji mbalimbali Mastaa kutoka nchi zinazoshiriki kinyang’anyiro hicho kwa mwaka huu.
Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA, wachezaji wenye majina yenye herufi “M” ndio wanaoongoza kwa idadi kubwa katika michuano hiyo ambao jumla yao ikiwa ni 85.
Miongoni mwa wachezaji hao ni mshambuliaji Lionel Messi kutoka Argentina, Thomas Mülar kutoka Ujerumani,John Obi Mikel kutoka Nigeria, Hossein Mahini kutoka Iran na  wachezaji wengine kutoka mataifa yanayoshiki finali hizo.
Majina mengine 807 ya wachezaji yapo katika herufi “A” hadi “Z” ukiyatoa yale ya herufi “M” ambapo  herufi A wapo wachezaji 68, B 69, C 57, D 56, E 21, 25, G 47, H 40, I wachezaji 17, J 42, K 42, L 30, N 17, O 23, P 40 na Q mchezaji mmoja, R 43, S 70, T 19, U wachezaji watano, V 37, W, 16, X  wachezaji wawili, Y na Z wachezaji 10.
Katika mashindano hayo kuna jumla ya nafasi 736 za wachezaji ambapo kuna magolokipa 96, walinzi 230, walinzi wa kati 250 na washambuliaji 160. 
Wachezaji hao wanatoka katika timu za mataifa ya Algeria, Argentina, Australia, Ubelgiji,  Bosnia na Herzegovina, Brazil, Cameroon, Chile, Colombia, Costa Rica, Ivory Coast, Croatia, Ecuador, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ghana.
Mataifa mengine yanayoshiki fainali hizo ni Ugiriki, Honduras, Iran, Italia, Japan, Jamuhuri ya Korea, Mexico, Uholanzi, Nigeria, Ureno, Urusi, Hispania, Switzerland, Uruguay na Marekani.
Wachezaji hao wanaounda timu za mataifa yao kwa kutokana na uraia wao aidha wa kuzaliwa au kujiandikisha na wanacheza mpira katika vilabu mbalimbali duniani.
Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA,  wachezaji 14 wanazechezea timu ya Bayern Muenchen,wachezaji 14 wanazechezea timu ya Manchester United, 13 Barcelona, 12 Chelsea, 12 Juventus,  12 Real Madrid,  12 SSC Napoli, 10 Liverpool, 10 Manchester City,  10 Paris Saint-Germai na  wachezaji 10 wanachezea timu ya Arsenal.
Vilabu vingine vilivyotoa wachezaji wanaoshiriki faina hizi ni Atletico Madrid wachezaji 9, FC Porto wachezaji 9,  FC Internazionale wachezaji 8,  AC Milan wachezaji 8,  Schalke 04 wachezaji 7, FC Zenit St. Petersburg wachezaji 7,  FC Dynamo Moscow  wachezaji 7,  SS Lazio wachezaji 7, Southampton FC wachezaji 7, VfL Wolfsburg wachezaji 7, Tottenham Hotspur wachezaji 6,  Newcastle United wachezaji 6, FC Basel wachezaji 6, Everton wachezaji 6,  CSKA Moscow wachezaji 6,  Borussia Dortmund wachezaji 6, AS Roma wachezaji 5, Feyenoord Rotterdam wachezaji 5, Fenerbahce SK wachezaji 5,  FSV Mainz 05 na  Galatasaray SK  zote zimetoa wachezaji watano kila mmoja.
Ili kuhakikisha timu za mataifa hayo zinakuwa na mafanikio wapo jumla ya makocha 32 wa timu za mataifa hayo ambao wanaongoza benchi la ufaundi kwa timu zao.
Fainali  mwaka huu zilianza 12 Juni na zinatarajiwa kuhitimishwa Julai 13 kwa kwa mechi ya fainali ambayo itaamua nani atatawazwa kuwa mwamba wa soka duniani baadya ya bingwa mtetezi Hispania kutolewa mapema katika mzunguko wa kwanza wa mashindano haya.
Mpaka sasa hadi kufikia kipindi hiki cha hatua ya pili ya timu 16 bora, miamba iliyofanikiwa kupenya katika hatua hiyo kutoka kundi A ni Brazil na Mexco, kundi B Uholanzi na Chile, kundi C ni Columbia na Ugiriki, kundi D Costa Rica na Uruguay, kundi E ni Ufaransa na Swirtzerland, kundi F ni Argentina na Nigeria, kundi G ni Ujerumani na Marekani na kutoka kundi H timu zilizopenya ni Ubelgiji na Algeria.
Kigenga cha hatua ya timu 16 bora kitapulizwa Juni 28 mwaka huukwa timu ya wenyeji wa mashindano Brazil kuvaana na Chile.
Timu nyingine zilizofuzu hatua hiyo ni Columbia ambao watacheza na Uruguay, Uholanzi watacheza na Mexco, Costa Rica watacheza na Ugiriki, Ufaransa watacheza na Nigeria, Ujerumani watacheza na Algeria, Argentina watacheza na Swirtzerland na kipenga cha mwisho katika hatua hii kitakuwa kati ya Ubelgiji ambao watavaana na Marekani hapo Julai Mosi mwaka huu katika dimba la Arena Fonte Nova, Salvador nchini Brazil.
Mataifa yaliyofuzu kushriki fainali za mwaka huu ni 32, ambapo imekuwa na fainali ya 19 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1930. Mataifa hayo yanatoka katika bara la Africa, Asia, Amerika ya kaskazini, Amerika ya kusini, Oceania na Ulaya.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI