Sunday, June 1, 2014

MCHINA AGUNDUA BAISKELI SANDUKU

Raia  wa China Ndugu  He Liang amegundua Sanduku baiskel
Raia wa China Ndugu He Liang amegundua Sanduku baiskel.
Ubunifu unazidi kurahisisha maisha Duniani ambapo raia mmoja wa China Ndugu He Liang amegundua sanduku ambalo lina matairi mawili lenye uwezo wa kwenda umbali wa Kilomita zisizopungua 60 kwa kasi ya Kilomita 20 kwa saa na linatumia nishati ya umeme ambayo ni betri.
Mgunduzi huyo ametumia miaka 10 kulitengeneza sanduku hili ambalo lina nafasi ya kutosha ya kuweka nguo ambapo likiwa tupu lina uzito wa Kilo 7. Sanduku hilo lina uwezo wa kubeba mtu mmoja na ikiwa ni baiskeli yenye ufanyaji kazi kama wa pikipiki.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI