MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Mh Joshua Nassari leo kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.
Kwa Mujibu wa Mh Nassari, sherehe hizo watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kwamba hakuna kadi.
"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!" alisema Nassari.
Nasari amesema watu zaidi ya 8000 kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa, Meru
0 comments:
Post a Comment