Sunday, May 18, 2014

WASTARA ALIPOVISHWA PETE HUKO UK...!!! TAZAMA PICHA ZOTE HAPA..!!!


 

Wastara akivishwa pete ya uchumba 
STAR mkubwa wa filamu nchini Tanzania Wastara Juma ambaye kwasasa yupo London Uingereza amevishwa pete ya uchumba huko na mwanaume anayeonekana hapo pichani. Wastara aliweka picha kadhaa kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii na wengine kudhani ni filamu mpya. Star mwenzake pia Riyama Ally ambaye wapo wote huko London nae aliandika "Ama kweli Mungu akitaka kukupa haandiki barua......,kila la kheri mama huu mwanzo mzuri kwako".

Alipoulizwa kama ni kweli au lah star huyu hakuwa na la kusema pengine kwa furaha na kuishia kujibu kwa ufupi kwa kusema "No comment" alipododoswa tena alijibu hivyo hivyo tena "No comment".

Wastara Monalisa, Riyama Ally na Cloud ni takribani wiki tatu sasa wapo London kwa mwaliko maalum na kucheza filamu inayoitwa Ughaibuni (Abroad) ambapo tayari wameanza kuishuti. Tungependa kuwatakia kila la kheri wawili hao. Angalia picha zaidi Wastara akivishwa pete hiyo..............
 
   
Chanzo: Swahiliworldplanet 

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI