Sunday, May 18, 2014

ARSENAL WALIPOTWAA UBINGWA KOMBE LA FA

BAO la dakika ya 108 la Aaron Ramsey limeipa Arsenal ubingwa wa Kombe la FA baada ya kuichapa Hull City 3-2 ikitoka nyuma kwa 2-0 Uwanja wa Wembley.Ramsey alifunga bao hilo akimalizia kazi nzuri ya Olivier Giroud na kuondoa uwezekano wa mchezo huo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti.
Arsenal waliuanza kichovu mchezo huo na kujikuta wanafungwa mabao mawili ndani ya dakika nane, Chester akianza kufunga la kwanza dakika ya nne na Davies akafunga la pili dakika ya nane.
Shujaa; Aaron Ramsey kushoto akiwa amejibwaga chini kushangilia bao lake la ushindi aliloifungia Arsenal katika fainali ya Kombe la FA usiku huu Uwanja wa Wembley. Kulia ni Jack Wilshere 
Wachezaji wa Arsenal wakiwa wamemlalia mfungaji wao bao la ushindi Aaron Ramsey 
Kocha Arsene Wenger akitoa maelekezo kwa vijana wake kabla ya kuanza kwa dakika 30 za nyongeza
Santi Cazorla aliifungia Arsenal bao la kwanza dakika ya 17 kwa shuti la mpira wa adhabu kabla ya Koscielny kufunga la pili dakika ya 72 na Ramsey la ushindi dakika ya 108.
Ushindi huo ni furaha kwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye hajatawaa taji lolote kwa miaka tisa.
Mara ya mwisho Arsenal walitwaa taji mwaka 2005, ambalo lilikuwa Kombe hilo hilo la FA wakiendeleza mafanikio ya msimu wa 2003-2004 walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Ngao ya Jamii.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Ramsey, Cazorla/Wilshere dk105, Ozil/Rosicky dk105, Podolski/Sanogo dk61 na Giroud.
Hull: McGregor, Chester, Bruce/McShane dk67, Davies, Elmohamady, Livermore, Huddlestone, Meyler, Rosenior/Boyd dk103, Quinn/Aluko dk74 na Fryatt.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI