Sunday, April 6, 2014

WADAU WA MUZIKI WA DANSI WAKUTANISHWA NA TBC KUJADILI CHANGAMOTO KATIKA MZIKI HUO

Wadau wa muziki wa Dansi katika picha ya pamoja
Wadau wa muziki wa dansi Asha Kigundula na mwandishi wa gazeti la mwananchi
Baadhi ya wasanii wa bendi mbalimbali wakiwa katika mdahalo wa muziki wa dansi kutoka kushoto ni King Kiki, Juma Ubao, Mafumo Bilali 'Bombenga' Kassimu Mapili na Waziri Ally
Wadau wa muziki wa dansi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika mdahalo
Baadhi ya wadau wa muziki wa dansi wakiwa katika meza kuu kushoto ni Mwani Nyangasa, Rose Chitara kushoto ni Muddy Muzungu
Baadhi ya wadau wa muziki waliojitokeza katika mdahalo wa muziki wa dansi kutoka kushoto ni , Deo Mutta Mwanatanga,Taasisi Masela na Super Nyamwela wa Extra Bongo 
Mwani Nyangasa kulia akiwa na Richard Mangustino
Wadau katika picha ya pamoja
Na mwandishi
WASANII wa muziki wa dansi pamoja na wadau mbalimbali wa mziki huo walikutanishwa na Shilika la utangazaji la Taifa TBC kwa ajili ya mdahalo wa kujadili mambo mbalimbali yanayohusu kuporomoka kwa mziki huu wa dansi nchini.
Mdahalo huo ulioratibiwa na Dakota Khamis anaetangaza kipindi cha nyumbani ni nyumbani umeleta hamasa kwa wasanii hao kufungua ukurasa mpya baada ya mada mbalimbali kujadiliwa wakati wa mdahalo huo. 
Mada zilizozungumzwa 
1. Sababu ya Kuporomoka kwa Muziki wa Dansi.
2. Mikataba na wajibu wa wamiliki wa bendi kwenye vifo na maradhi
3. Ushirikiano wa Wamiliki wa bendi
4. Maadili ya uchezaji kwa wanenguaji.
wanamziki hao ambao mara nyingi walikuwa wakilalamikia vyombo vya habari hususani tv na radio kutokupiga nyimbo zao na kuendelea kuwapa muda mrefu wasanii wa kizazi kipya ambao mara nyingi nyimbo zao hazina ujumbe mahususi na uandishi mzuri.
Baadhi ya waliokuwepo; Dacota Khamis, Rose Chitallah, Chacha Sinda, Mody Muzungu, Chiki Mchoma, Sunday Mwakanosya, William Kaijage, Kassim Mapili, Abdul Salvador, Deo Mutta Mwanatanga, Richard Mangustino, Rajabu Mhamila 'Super D', Asha Baraka, Ally Choki, Mwani Nyangasa, Asha Kigundula, King Kiki, Hussein Jumbe, Saidi Kibiriti, Waziri Ally, Juma Ubao, Mafumu Bilali, Othman Suka na Taasisi Masela.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI