Saturday, April 26, 2014

VAN GAAL AMTEUA KLUIVERT KOCHA MSAIDIZI WAKE MAN UNITED

KOCHA Luis van Gaal anajiandaa kumchukua Patrick Kluivert akawe msaidizi wake atakapojiunga na Manchester United.
Kwa mujibu wa gazeti la De Telegraaf na Uholanzi, ambalo lina ukaribu na kambi ya Van Gaal, kocha huyo tayari amejihakikishia kazi Old Trafford, amapo ulifanyika mkutano siku chache zilizopita baina ya wawakilishi wa Van Gaal na United.
Makocha wapya Old Trafford? 
Louis van Gaal atamchukua 
Patrick Kluivert akawe Msaidizi wake 
Man United
Gwiji: Kluivert alikuwa mchezaji wa 
Van Gaal katika klabu za Ajax na Barcelona 
United imekanusha madai ya kufikia makubaliano, lakini gazeti pia limesema Kluivert - kwa sasa anafanya kazi chini ya Van Gaal katika timu ya taifa ya Uholanzi- anaweza kurithi mikoba iwapo Van Gaal ataondoka.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi alicheza chini ya Van Gaal katika klabu za Ajax na Barcelona kabla ya kusajiliwa na Newcastle mwaka 2004.
Kocha wa makipa, Frans Hoek na mchua misuli, Jos van Dijk pia wanatajwa kuwamo katika timu ya Van Gaal ya benchi la Ufundi atakayohamia nayo United.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI