Sunday, April 27, 2014

TFF YATAKIWA KUWAENDELEZA VIJANA WA ARS

Baadhi wa washiriki wa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya darasani kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Shirikisho la mpira wa miguu nchi (TFF), imetakiwa kuhahakisha inawalea vijana waliopata nafasi ya kushiriki kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars ili waweze kulisadia taifa kwa hapo baadae.
Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa Abeid Musiba na Zamoyoni Mogella walitoa kauli hiyo kwenye uwanja wa Azam wa Complex jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kuwatembelea washiriki wa kliniki ambayo ina washiriki 72 kutoka nchi 12 Barani Afrika huku Tanzania ikiwakilishwa na washiriki 19.
‘Ninayo furaha kuona mwekezaji kama Airtel kwa kushirikiano na Klabu ya Manchester United ya Uingereza, zimejitokesa kusaidia maendeleo ya soka, hatuna budi kuhakikisha vipaji hivi vinaendelezwa pamoja na kukuzwa zaidi,’ alisema Mogella.
Mogella alisema kuwa hana uhakika serikali imeweza kutoa miundo mbinu inayowezesha michezo kufanyika, hivyo jukumu la kuhakikisha vipaji na elimu wanayoipata vijana hawa inabaki kwa TFF.
Kwa siku za karibuni serikali imekuwa ikitoa mazingira kwa wawekezaji kama hawa ili waweze kufanya kazi yao vizuri. Na kwa maana hiyo nayo watahamasika na kuwekeza zaidi kwenye sekta za michezo. Wakati sisi tunacheza mambo kama hayo hayakuwepo. Alisema Musiba.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Yanga Africans alisema Tanzania na hata baadhi ya nchi za Afrika zilikuwa hazifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa sio kwa sababu hazina vijana wenye vipaji vya soka, bali ni kutoka na ukosefu wa programu madhubuti za kuendeleza vijana ambao ndio muhimili wa maendeleo ya soka.
Wachezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella na Abeid Mziba, wakisalimiana na washiriki wa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella, akiongea na washiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars wakati walipowatembelea kwenye kliniki hiyo inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI