Sunday, April 27, 2014

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR ZAFANA UJERUMANI: PROFESA MUHONGO AWA MGENI RASMI

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akiingia katika ukumbi wa Deustche Bank uliopo Berlin, Ujerumani kabla ya kuzindua rasmi sherehe za jubilee ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulia ni balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe. Philip Marmo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza na baadhi ya wajumbe waliohudhuria sherehe hizo
Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza kabla ya kuanza kwa sherehe hizo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akibadilishana mawazo na balozi wa heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Hamburg Petra Hammelmann. Kulia ni mume wa balozi huyo Bw.Bertold Zink.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) (wa pili kutoka kulia) akiwa amesimama kwa heshima na wajumbe wengine wakati wimbo wa taifa ukipigwa na kikundi cha ngoma za sanaa cha Jeshi la Wananchi Tanzania
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ili afungue maadhimisho hayo
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akifungua sherehe hizo
Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa Palamagamba Kabudi (wa tatu kutoka kulia) akichangia mjadala juu ya historia ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ujerumani wakati wa maadhimisho ya sherehe hizo
Timu ya wataalamu kutoka Tanzania waliohudhuria sherehe hizo wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Nchini Ujerumani Mhe. Philip Marmo (wa kwanza kulia)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI