Waokoaji wamefaulu kuingia ndani ya feri iliyozama
NAIBU wa tatu wa nahodha wa ferri iliyozama ''Sewol'' ndiye aliyekuwa usukani wakati feri hiyo ilipozama.
Uchunguzi wa kimsingi umebaini.
Nahodha mkuu haijabainika alikuwa wapi wakati wa tukio ila inadhaniwa feri hiyo iligonga mwamba na kupinduka kwa haraka baada ya shehena yake kuegemea upande mmoja.
Wachungizi sasa wanaelekeza juhudi zao kubaini kwanini Nahodha wa Sewol hakuwa kwenye usukani na pia kwanini baada ya tukio la kwanza abiria walikanywa wasiruke baharini ilikuokoa nafsi zao kama ilivyodesturi chombo
kikigonga mwamba ?
Kiongozi wa Mashtaka ya umma nchini Korea bwana Park Jae-Eok amesema kuwa nahodha mkuu Lee Joon-seok,atakuwa na swali la kujibu.(P.T)
Kufikia sasa abiria 270 waliokuwa ndani ya feri hiyo hawajulikani walipo asilimia kubwa kati yao wakiwa ni wanafunzi waliokuwa wakieleka katika kisiwa cha Jeju kwa safari ya masomo.
Watu 26 pekee ndio wamedhibitishwa kufariki kufikia sasa, huku 179 wakiokolewa.
Muundo wa feri iliyozama
Makundi ya waokoaji wamefanikiwa kuingia ndani ya feri hiyo kwa mara ya kwanza leo asubuhi baaha ya kutoboa shimo upande wa juu wa chombo hicho kilichozama.
Waokoaji walikuwa wameshindwa kuingia ndani ya feri hiyo baada ya bahari kuchafuka.
Mamia ya jamaa na marafiki ya wahasiriwa wamelalamikia ukosefu wa habari za uokaji .
Wengi wamekuwa wakivumilia hali mbaya ya hewa wakiomba kuruhusiwa kusubiri wapendwa wao ufukweni.
0 comments:
Post a Comment