Thursday, April 17, 2014

MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA ZAONDOKA NA MIUNDOMBINU YA RELI NJIA YA DAR-TANGA-MOSHI ENEO LA MING’ONG’O KM 4 TOKA STESHENI YA RUVU

Sehemu ya njia ya reli katika eneo la Ming’ongo ikiwa inaning’inia baada ya tuta kusombwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Kipalo Amani Kisamfu pamoja na wakurugenzi kutoka Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo kuona athari kubwa iliyotokea kwenye njia ya reli. 
Aidha, katika njia hiyo kilomita kumi na nane za njia ya reli zimeaharibiwa na mvua hizo zinazoendelea kunyesha katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Reli, Wizara ya Uchukuzi, Bw. Festo Mwanjika (wa pili kutoka kulia) akiangalia uharibifu mkubwa uliotokea kwenye njia ya reli katika eneo la Ming’ong’o kilomita 4 kutoka Stesheni ya Ruvu, alipotembelea eneo hilo kujionea moja kati ya sehemu kumi na nane zilizoharibiwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. 
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Uchukuzi

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI