Saturday, April 5, 2014

MICHAEL SATA, "ULAYA NDIO CHANZO CHA MACHAFUKO AFRIKA"

RAIS Michael Sata wa Zambia amesema kuwa, nchi za Ulaya ndio chanzo cha migogoro katika nchi za bara la Afrika.
Rais Sata ameyasema hayo katika kikao cha viongozi wa Ulaya na Afrika, mjini Brussels, Ubelgiji na kuongeza kuwa, uzalishaji wa silaha zisizohitajika na kuyapatia silaha makungi ya waasi katika nchi tofauti za Kiafrika, umepelekea kuongezeka wimbi la machafuko katika nchi za bara hilo. Rais wa Zambia ameenda mbali zaidi na kusema kuwa, hivi sasa watoto wengi wanaoingizwa jeshini, licha ya umasikini mkubwa unaowakabili, wanabeba silaha zenye thamani kubwa ambazo zimetengenezwa na nchi za Ulaya. Swali la msingi ni kwamba, watoto hao wanapata wapi fedha za kununulia silaha hizo licha ya umasikini walionao?, amehoji Rais Michael Sata wa Zambia.
Karibu kila siku raia wa kawaida katika nchi mbalimbali barani Afrika wakiwamo wanawake na watoto hupoteza maisha yao na kuwa wakimbizi kutokana na machafuko yanayotokea barani humo.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI